“Jifunze Kijapani” kinatolewa na NHK WORLD. NHK WORLD ni matangazo ya kimataifa ya NHK. NHK inaendesha matangazo ya kimataifa ya televisheni, redio na mtandao wa intaneti, kwa pamoja zinajulikana kama NHK WORLD.
Katika kila somo, unaweza kujifunza misemo muhimu kwa njia ya sauti. Hadi utakapofika mwisho wa mfululizo wa masomo haya, utakuwa unajua misemo ipatayo 50 !